Nafasi Ya Matangazo

September 20, 2021

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Abdalla Said Hamad (kushoto) akimkabidhi barua ya uteuzi mgombea wa Chama Cha AAFP Hamad Khamis Mbarouk, baada ya kurejesha fomu na kutimiza masharti ya uteuzi
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Abdalla Said Hamad (kushoto) akimkabidhi barua ya uteuzi mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo, Mohamed Said Issa  baada ya kurejesha fomu na kutimiza masharti ya uteuzi.
 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Abdalla Said Hamad  akimkabidhi barua ya uteuzi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mbarouk Amour Habib baada ya kurejesha fomu na kutimiza masharti ya uteuzi
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Abdalla Said Hamad (kushoto) akimkabidhi barua ya uteuzi mgombea wa Chama Cha Wananchi CUF, Salama Khamis Omar baada ya kurejesha fomu na kutimiza masharti ya uteuzi.
*********
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewateua Wagombea vinne Kati ya vitano waliochukua fomu kuomba uteuzi wa kuwania Ubunge Jimbo la Konde Wilayani Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Visiwani Zanzibar.

Awali vyama vinne vya Siasa vilijitokeza kuchukua fomu za kuwania Ubunge katika Jimbo la Konde.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Abdalla Said Hamad  amewataja  Wagombea na vyama vilivyorejesha fomu na kupata uteuzi kuwa ni Mbarouk Amour Habib wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamad Khamis Mbarouk wa Chama cha AAFP, Salama Khamis Omar wa Chama Cha Wananchi CUF na Mohamed Said Issa wa ACT Wazalendo. 

Zoezi la utoaji fomu kuwania kiti cha Ubunge Jimbo la Konde lilianza tarehe 13 na kufikia ukomo leo Septemba 19,2021. 

Hamad mesema mgombea wa Chama cha NCCR Mageuzi, Abdirahim Ali Slum hakurejesha fomu zake hadi muda wa uteuzi ulipomalizika Saa 10 kamili jioni hivyo ameenguliwa katika kinyang'anyoro hicho.

Vyama vyote vinne vilivyoteuliwa vimekabidhiwa barua ya uteuzi na endapo Hadi ikifika Saa 10 jioni Septemba 20,2021 muda wa mapingamizi utakapo malizika wagombea hao wataruhusiwa kuanza kampeni za Uchaguzi. 
Jimbo la Konde linafanya uchaguzi Mdogo Oktoba 9,2021 pamoja na Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga na Kata tisa za Tanzania Bara.
Posted by MROKI On Monday, September 20, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo