Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, wakiwa katika picha mbele ya Gari aina ya Volkswagen mara baada ya kutembelea kwenye Kiwanda cha kutengenezea Magari CFAO MOTORS Mjini Kigali Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti,2021.
-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 03 Agosti, 2021 amehitimisha Ziara yake ya siku mbili nchini Rwanda kwa kutembelea viwanda vitatu na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na viwanda hivyo.

Katika kiwanda cha kwanza cha Inyange kinachotengeneza vinywaji, Mhe. Rais Samia akiwa na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wamejionea shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na maji ya kunywa, maziwa na juisi.

Aidha, Mhe. Rais Samia pia ametembelea kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi cha Mara Phone na kujionea hatua mbalimbali za utengenezaji wa simu kuanzia hatua ya awali hadi kukamilika kwake.

Pia Mhe. Rais Samia ametembelea kiwanda cha uunganishaji magari cha Volkswagen kilichopo nchini humo na kujionea hatua mbalimbali za kuunganisha magari hayo ambayo huuzwa nchini humo.

Mhe. Rais Samia amewaagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo ili kutumia fursa zilizopo katika viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuwauzia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania.

Mhe. Rais Samia ameagana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali na kurejea Jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo.

Posted by MROKI On Wednesday, August 04, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo