Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2021

 

Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zilizoenea katika mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni zinazodai kwamba Waheshimiwa Wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao.

Tunapenda kuujulisha umma kwamba  Waheshimiwa Wabunge kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa umma  na Viongozi wa Kisiasa wanakatwa kodi zote stahiki kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kodi ya mapato (PAYE) inayokatwa kwenye mishahara ya Wabunge.

Hivyo tunaomba umma upuuze taarifa hizo na tunatoa wito kwa Vyombo vya Habari hususan mitandao ya kijamii kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Mamlaka husika ili kupata ukweli kabla ya kutoa taarifa kama hizi.

Imetolewa na:     Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,

 Ofisi ya Bunge,

 S.L.P 941,

 DODOMA.

 

3 Agosti, 2021.


Posted by MROKI On Tuesday, August 03, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo