Nafasi Ya Matangazo

July 28, 2021

 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (kulia aliyevaa kofia) akikagua neneo panapojengwa majengo ya wodi tatu za hospitali ya Mtowisa wilaya ya Sumbangwa.Akiwa kwenye eneo hilo ameonesha kutoridhishwa na kazi za ujenzi huo na kuagiza kusitishwa kwa ujenzi hadi mapungufu ya kitaalam kwenye ujenzi wa msingi yatakaporekebishwa.Serikali imetoa shilingi Milioni 500 kwenye mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (aliyevaa kofia) akisoma barua ya malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Mfinga  jana (27.07.2021)  mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kasekela wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akishuka mlimani kutoka kukagua tenki la maji wakati alipotembelea mradi wa  maji Kasekela kitongoji cha Kipenzi Kata ya Mfinga wilaya ya Sumbawanga jana. Akiwa kwenye eneo hilo alitoa agizo la viongozi wa kijiji kudhibiti matukio ya uchomaji moto msitu yanayoendelea .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba (kulia) jana wakiwa kwenye eneo inapojengwa moja kati ya shule mpya ya kata ya Kalumbaleza wilaya ya Sumbawanga. Akiwa hapo Mkirikiti ametoa agizo kwa halmashauri kukamilisha ujenzi huo kaba ya ifikapo mwezi Desemba waka huu ili wanafunzi waanze kusoma.

Posted by MROKI On Wednesday, July 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo