Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2019


Wafanyakazi wa Tanesco wakishiriki katika maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa jijini Dodoma. 
 MACHI 8 ya kila mwaka ni siku ya wanawake Duniani, wanawake wengi hasa wa mijini huadhimisha siku hii kwa maandamano na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidia wanawake wenzao katika jamii.

Maadhimisho ya mwaka huu yana kauli mbiu inayosema “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”

Rais John Magufuli wakati akiagana na mgeni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda alituma salamu za heri kwa wanawake wote nchini.

Rais Magufuli amewatumia salamu za pongezi wanawake wote Tanzania na kusema serikali ina thamini na kutambua mchango mkubwa wa Wanawake wa Tanzania.   
Wanawake wa Shirika la Umeme nchini TANESCO ni miongoni mwa wanawake waliojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hii sawa na wanawake wenzao katika maeneo mbalimbali nchini na Duniani.

Tanesco makao Makuu jijini Dodoma ilishiriki maadhimisho hayo kwa kuanza na maandamano na kisha katika shughuli zingine zilizopangwa kufanyika katika maadhimisho hayo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde amewaasa wanawake kudumisha upendo na umoja katika kushiriki shughuli za maendeleo nchini kwa kushikamana pamoja bila kujitenga.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2019 katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.

Naibu Waziri alibainisha miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanawake ni pamoja na kukosekana kwa umoja, upendo na ushirikiano ambao unawaga katika makundi na kusababisha wanawake kutokuwa na maendeleo ya pamoja.

“Niseme ukweli japokuwa hamtaupenda kwa leo, miongoni mwa sababu zinazowakwamisha katika kuendelea ni tabia ya chuki miongoni mwenu, umbeya na makundi yasiyoleta tija za kimaendeleo,”alieeza Mavunde

Aliongezea kuwa, wanawake wanapaswa kubalidi mitazamo na tabia ambazo zinawaga na kuondoa upendo kati yao na kujikuta wanajitenga hivyo, kupunguza nguvu kazi ya pamoja katika uzalishaji na kuchangia kusuasua kwa maendeleo yao.

Aidha Mavunde alieleza kuwa, kwa kuzingatia mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo nchini ni vyema wakaishi kwa upendo na umoja ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.

“Kimsingi wanawake ni nguzo imara inayotegemewa na Taifa kwa kuzingatia uthubutu na namna Mungu alivyowapa roho ya kuvumilia na kuwaamini katika utendaji wenye uadilifu,”alisisitiza Mavunde.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akihutubia wanawake walioshiriki wakati wa Maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani Mchi 8, 2019 katia Viwanja vya Mashujaa Dodoma yenye Kauli mbiu isemayo Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”


 Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika maandamano ya kuadhimishi siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Mashujaa Dodoma.
 Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho hayo.
Kikundi cha bendi ya JUKIMSI wakionesha umahiri wao wa kuimba wakiwa katika gari maarufu kwa jina la “kijiko” wakati wa maadhimisho hayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiangalia moja ya mfuko ulioshoinwa kwa kitengo na kikundi cha Angel kutoka Dodoma wakati wa maadhimisho hayo.
Posted by MROKI On Friday, March 08, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo