Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2018

WAVAMIZI wa kimtandao wamevamia akaunti binafu ya mtandao wa Instagram ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete na kumfanya ashindwe kuingia katika mtandao huo.

Mbali na kumzuia Mbunge huyo kuingia katika akaunti yake hiyo, pia wavamizi hao wameandika ujumbe ambazo ni zakumchafua Mbunge huyo.

Father Kidevu Blog, imewasiliana na Mbunge huyo na kabla ya kusema lolote alijibu kwa kifupi, "Nimesikitishwa sana na hili jambo lililotokea leo".

Ridhiwani ambae pia ni Mtoto wa Rais Mstaafu awamu ya nne, Jakaya Kikwete alisema kuwa watu hao wameingilia mtandao wake wa Instagram na kumzuia asiingie kwenye akaunti yake.

"Watu wameingilia Ukurasa wangu wa Instagram na kunizuia nisiingie kwenye account yangu. Lakini jambo baya zaidi wanalolifanya ni kuandika vitu au maneno ambayo hata sijawahi na sitamani kuyasema," alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa kitendo hicho kimemshangaza sana na hajajua nani aliyefanya hivyo na snia hasa ilikuwa ni nini, huku akisema kamwe hawatafanikiwa.

"Nimeshangazwa sana na hili na sijui nia ya kufanya hivyo ni nini? Malengo yenu hamtafanikiwa,"alisema. 

Ridhiwani alisema kuwa wakati hayo yakitokea yeye alikuwa katika vikao vya halamashauri kupanga bajeti za Halmashauri ya Chalinze. 

Pia alidai kuwa manna na matukio yaliyoandikwa katika mtandao wake huo hayajawahi kutokea na kuwaomba watu wake na marafiki zake kuwa watulivu.

"Naomba utulivu katika kipindi hicho ambacho wataalamu wanafanya kazi ya kurudisha Ukurasa huu mikononi mwangu".
Posted by MROKI On Tuesday, January 23, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo