Nafasi Ya Matangazo

December 10, 2017

Magwiji wa kuonyesha michezo kote barani Afrika – SuperSport imethibitisha rasmi kupata idhini ya kuonyesha  moja ya michuano maarufu kabisa ya soka ulimwenguni.
 
Kombe la UEFA ambapo sasa michuano hiyo itaonekana mubashara kupitia DStv na hivyo kuwawezesha mamilioni ya watazamaji kote barani Afrika kushuhudia michezo hiyo.

Hivi karibuni, SuperSport ilishiriki katika zabuni ya kupata idhini ya kuonyesha michuano hiyo na hatimaye kuthibitisha kupata idhini ya kuendelea kuonyesha michuano hiyo kwa miaka mitatu ijayo kuanzia msimu wa 2018/19.

“Hii ni siku ya Furaha na muhimu sana kwa SuperSport na wateja wetu wote wa DStv” amesema Mtendaji Mkuu wa SuperSport Gideon Khobane na kuongeza kuwa michuano ya UEFA ni moja ya mashindano makubwa na yanayoshirikisha timu maarufu na wachezaji nyota wengi sana hivyo itakuwa ni burudani ya aina yake kwa watazamaji wa DStv kote barani Afrika. 

Amesema kama kawaida, kupitia DStv, watazamaji wataona michuano hiyo mubashara tena kwa muonekano wa kiwango cha juu.

Idhini waliyopata SuperSport ni pamoja na urushaji matangazo katika Televisheni, simu na kupitia internet kwa ujumla.
Posted by MROKI On Sunday, December 10, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo