Nafasi Ya Matangazo

September 09, 2017 Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu,  Emanuel Maganga, alisema Wakimbizi akiwa amembeba mmoja wa watoto wa wakimbizi kutoka Burundi wakati wa kuwarejesha makwao kwa hiati ambapo wakmbizi 301 wameanza kurejea  katika Mkoa wa Ruyigi na Bujumbur.
 Viongozi mblimbali kutoka Serikali ya Tanzania na Burundi wakimsikiliza Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laizer, ambaye aliwaeleza kuwa kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na kati ya hao watu 12,000 wameomba kurudishwa makwao.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
UTEKELEZAJI wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam baina ya pande tatu za serikali ya Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakurejesha wakimbizi wa Burundi  wapatao 12,000 umeanza utekelezaji.

Katika utekelezaji huo kwa awamu ya kwanza Wakimbizi 301  waliokuwa wakiishi katika kambi ya Nduta Wilayani Kibondo, walioomba kerejea Nchini mwao kwa hiyari wameanza kurejeshwa makwao baada ya kujiridhisha kwa kuwepo hali ya amani. 

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi Wakimbizi hao kwa Naibu waziri wa mambo ya ndani ya Nchini Burundi , katika Mpaka wa Mabamba  Wilayani Kibondo, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu,  Emanuel Maganga, alisema Wakimbizi wanaoanza kurejea ni kutoka  Mkoa wa Ruyigi familia 60 na Bujumbura familia 37 .

Alisema kikao walicho kaa wiki iliyopita  cha pande tatu kiliamua Wakimbizi waliomba kurejeshwa Nchini mwao  warejeshwe na kwasasa wao kama serikali ya Tanzania wameanza kuwarejesha na kuwakabidhi kwa serikali ya Burundi  wakimbizi 301 na hadi mwezi wa tisa wanatarajia kuwarejesha wakimbizi 6,000 na wengine watawarejesha mwezi wa kumi na mbili mwaka huuu.

Aidha Maganga aliwaomba Wakimbizi hao kuanza kujitokeza kurejea mapema na wasisubiri kuondoka kwa mrundikano hali inayoweza kuwapa ugumu katika usafirishwaji hivyo waanze kuondoka mapema.

Mratibu wa Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laizer, alisema kwasasa wanajumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 127,715 na kati ya hao watu 12,000 wameomba kurudishwa makwao na kuchelewa kurudishwa kuna pelekea sasa hali ya usalama kuwa si nzuri kwani kunawepo na vitendo vya vurugu za mara kwa mara kutoka kwa wakimbizi hao wanaotaka kuondoka.

"Urejeshwaji wa Wakimbizi hawa utasaidia kuwepo na usalama na amani katika kambi maana kuna wakimbizi wengi walikuwa wakiomba kurejeshwa kwao ninaamini hatua hii itasaidia kuwapa nguvu wakimbizi wengine kuendelea kuamini kuwa Nchini mwao kunaamani na zoezi hili litakuwa muendelezo kwa kambi zote", alisema Tony.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi  ya Burundi ,Therence Ntahiraja alisema wao kama Viongozi wa Burundi wamejipanga ipasavyo katika kuwapokea Wakimbizi na Watawakabidhi mali zao kama walivyokuwa mwanzoni na Watawapatia Maeneo ya kufanyia shughuli zao ilikuweza kuendesha maisha yao kama ilivyo kuwa mwanzo.

Alisema kwasasa Nchi ya Burundi ina amani na kuwaomba wakimbizi wote warejee Nchini mwao iliwaweze kufanya shughuli za maendeleo na kuhakikisha Nchi yao inakuwa kiuchumi.

Nao baadhi ya Wakimbizi waliokuwa wakirejea Nchini mwao, akiwemo  Isabera Niyonkuru  walisema Wanafuraha sana kurejea Nchini mwao na hatua hiyo itawawezesha kufanya shughuli mbali mbali na kuweza kuzitunza familia zao na kuepukana na kuwa wakimbizi.

" tunafurahi sana kuona serikali ya Tanzania imetutunza kwa kipindi chote tulichoishi Nchini humo tunawashukuru sana, tunaamini tunaporejea nyumbani kwetu tutapokelewa na kuishi kwa amani na tunaomba wasichoke kutusaidia tutakapokuwa na matatizo", alisema Niyonkuru.
Posted by MROKI On Saturday, September 09, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo