Nafasi Ya Matangazo

July 24, 2017

Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake Nelson Mbuya (wa pili kushoto), Stephano Huche na Joseph Panga(kulia)  wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli.  Wanariadha mbalimbali wameweka kambi jijini Arusha ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya dunia. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake Nelson Mbuya (katikati) na Joseph Panga  wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli.  Wanariadha mbalimbali wameweka kambi jijini Arusha ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya dunia. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London
Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taif ya riadha inayojiandaa kushieiki mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake wa timu ya taifa itakayoshiriki Mashindano ya Riadha ya Dunia jijini London wiki ijayo Ezekiel Ng’imba (katikati) na Said Makula wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
 ***************
Balozi maalum wa DStv na moja ya wanariadha wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka huu yatakayofanyika mwei ujao jijini London Alphonce Simbu, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani imejiandaa vizuri
Akizunngumza wakati wa ziara maalum ya Afisa muandamizi wa DStv Johnson Mshana katika kambi hiyo iliyopi Ilboru Arusha ambapo pia alishuhudia mazoezi ya timu hiyo, Simbu alisema kuwa yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanaleta medali nyumbani katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika mapema mwezi Agosti.
 “Tumejiandaa vizuri na tunamatumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi mazito na inaonekana vijana tuko sawasawa kupambana katika mashindano hayo” alisema Simbu
Naye meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana ambayo alitembelea kambi hiyo na kasha kushiriki katika mazoezi amesema Kampuni yao imefurahishwa sana na mwenendo wa kambi hiyo pamoja na timu nzima. “Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi ya timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii niyo sababu iliyotusukuma DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya Taifa itakayokwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania tushuhudie medali zikija nyumbani”
Amesema baada ya DStv kuanza kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita, wameshuhudia mafanikio makubwa sana. Ambayo yamewatia moyo sana kuamua kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi timu ili hatimaye iweze kufanya vizuri zaidi na kulikwakilisha vyema taifa kwenye michuano ya kimataifa.
“Tulianza na Simbu, amefanya vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi kwa timu yetu ya Tanzania na tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv ilionyesha mubashara Mumbai Marathon tukamuona Simbu akishinda, Tukaonyesha Mubashara London Marathon, tukaona Simbu akivunja rekodi yake, na tutaonyesha mubashara Mashindano ya Dunia Mwezi Agosti, ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua medali kedekede na kuliletea taifa letu sifa kubwa” alisema Mshana kwa kujiamini
Naye Kocha wa timu hiyo Francis John, amesema kazi kubwa imefanywa na makocho wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kwama  ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi yao kwenda vizuri. Amesema wanatarajia kuwa wanariadha hao watafanya vizuri  kwani hata mmoja wao aliyekuwa na matatizo ya magoti sasa anaendelea vizuri na bila shaka atasiriki vizuri kwenye mashindano.
Amesema jumla ya wachezaji saba  wakiwemo wanawake watatu na wanaume wane watashiriki Failuna Abdi  atashiriki mita 10,000 Gabriel Gerald mita 5,000 na  watano watashiriki marathon kamili ya kilomita 42 ambao ni Magdalena Krispin, Saraah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba na Alphonce Felix Simbu.
Timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo inatarajiwa kuagwa na kukabidhiwa bendera jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai na Mashindano hayo yanaanza tarehe 4 Agosti 2017.
Posted by MROKI On Monday, July 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo