Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2017



Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi mashuka kwa Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija Kopa na kulia ni Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni mabalozi maalum wa DStv. Hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo hicho ambapo vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vikiwemo vyakula, mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi King’amuzi cha DStv kwa Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija Kopa na kulia ni Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni mabalozi maalum wa DStv. Hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo hicho ambapo vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili vikiwemo vyakula, mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa



KAMPUNI ya Multichoice Tanzania imetoa zawadi ya sikukuu ya Idi kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam. Msaada huo wa vyakula na vifaa mbalimbali umekabidhiwa kwa kituo hicho na Meneja Operesheni wa Multichoice Baraka Shelukindo katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo ambayo pia ilihudhuriwa na mabalozi kadhaa wa DStv akiwemo malkia wa taarab Khadija Kopa na muigizaji maarufu wa filamu Riyama Alli.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Shelukindo amesema kwa takriban miaka mitano mfululizo Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho kwa mambo mbalimbali.  Amesema wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa malezi ya watoto waishio katika mazingira magumu ni jukumu la kila mtu na kila taasisi. 

“Tunatambua kuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu moja ama nyingine wamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni ndugu zetu, watoto wetu, na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo kuwasaidia ni jukumu letu”

Amesema mbali na kwamba Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho mara kwa mara kwa kuwapa vyakula na mahitaji mengine, lakini pia waliamua kufadhili uanzishwaji wa mradi wa ushonaji ambao unakisaidia kituo hicho katika kujiingizia kipato. 

“Tunajua kuwa chakula, malazi na mambo mengineyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya vijana wetu, lakini pia tuliona ni busara kuwawekea kamradi japo kadogo ambako wataweza kujipatia kipato. Tumefurahi sana kuona mradi huu unaendelea na tunaamini kuwa  wataweza kuuendeleza na kuukuza ili uwasaidia Zaidi.” Alisema Shelukindo.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho Mama Kuruthum Juma ameishukuru Multichoice kwa msaada wao wa mara kwa mara kwa miaka mingi sasa. Amesema kitendo cha Multichoice kukisaidia kitua hicho kwa mambo mbalimbali hususan mradi wa ushonaji kumewasaidia sana katika kujipatia kipata japo kusaidia gharama za uendeshaji kituo hicho ambazo ni kubwa.

“Kwa kweli gharama za uendeshaji kituo ni kubwa sana na kama mnavyofahamu watoto wanaolelewa hapa hawana uwezo na wengi wao hawana wazazi, hivyo ni jukumu letu kuwalea, kuwapa matibabu, na pia kuwasomesha, hili kwa kweli ni jukumu kubwa na tunahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali” alisema Mama Kuruthum

Amesema idadi ya watoto imekuwa ikiongezeka lakini kituo hakina uwezo mkubwa kutokana na ufinyu wa eneo na bajeti hivyo akawaomba wadau wengine kuangalia uwezekano wa kukisaidia kituo hicho ili kiweze kuhudumia watoto wengi Zaidi.

Naye Malkia wa Taarabu – Khadija Kopa amesema amefarijika sana kuona Multichoice inawajali watoto hususan wale waishio katika mazingira magumu ambao aghalabu husahaulika na jamii. 

“Kwakweli Multichoice wamefanya jambo la maana sana. Ni vyema tukaunganisha nguvu zetu kuwalea hawa watoto wetu kwani nao wana haki kama watoto wengine” alisema Kopa.

Naye muigizaji Riyama Ali amepongeza jitihada zinazofanywa na Multichoice pamoja na uongozi wa kituo cha Almadinna katika kuwasaidia watoto hao. “Watoto hawa ni hazina ya taifa. 

Tukiwasaidia hawa wakakua vizuri, wakapata elimu nzuri, kesho na keshokutwa tutapata wabunge humu, mawaziri, wakurugenzi, wanamichezo, wasanii na kadhalika. Tushirikian kuwale na hili ni jukumu letu sote na ni kitu kinacholeta Baraka” alisema Riyama.

Kituo cha Al-Madinnah Orphanage Centre kilianzishwa mwaka 2004na kwa hivi sasa kituo hicho kinahudumia jumla ya watoto 65 ambapo 40 kati yao ni wavulana na 25 wasichana na wengi wao ni wanafunzi wa shule za msingi.
Posted by MROKI On Thursday, June 22, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo