Nafasi Ya Matangazo

April 15, 2017

 
Kocha mchezaji wa timu ya Viongozi mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akionesha ufundi wake wa kutuliza mpira wakati akiwanoa wachezaji wake. Makalla pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
KATIKA hali ya kudumisha umoja, ushirikiano na amani katika mkoa wa Mbeya, viongozi wa serikali mkoani humo na viongozi wa dini wameaandaa mtanange wa mpira wa miguu ambao utazikutanisha timu hizo mbili.

Kocha mchezaji wa timu ya viongozi wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla ameiambia Daily News-Habarileo Blog kuwa tayari timu yake ipo kambini ikijifua kwa mchezo huo wanaotaraji uwe wa vuta ni kuvute kutokana na pande zote mbili kukamiana vilivyo.

Makalla amesema timu yake imeweka kambi katika uwanja wa maafande wa Magereza Mjini Mbeya wakiendelea na mazoezi ya aina mbalimbali ili kukiwezesha kikosi chake kuibuka na ushindi.

"Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya tunataraji kushuka dimbani kumenyana na viongozi wa dini. Mchezo huu tumepania kuutumia kulipiza kisasi maana miaka miwili iliyopita tulikutana na timu hiyo na kutuchapa mabao 2-0," alisema Makalla.

Alisema mchezo huo utakuwa wa aina yake na tayari mashabiki wengi wa soka katika mji wa Mbeya na Viunga vyake wanausubiri kwa hamu mchezo huo. 

Makalla alisema hadi hivi sasa kikosi chake kipo vizuri na anauhakika wa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya viongozi wa dini hivyo kuwataka wajipange vyema kwa mazoezi na dua ili waweze kuchomoka katika uwanja wa sokoine.

Misimu kadhaa Amos Makalla alipata kukinoa na kuchezea kikosi cha Moshi Veterans ya Mkoani Kilimanjaroa mabko alikuwa Mkuu wa Mkoa huo.
Posted by MROKI On Saturday, April 15, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo