Nafasi Ya Matangazo

January 15, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Kanali Marko Gaguti  akiwafariji wakazi wa kijiji cha Mnyegera ambapo upepo mkali ulitokea huko na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13.
Kanali Gaguti akitembelea makazi yaliyoathiriwa.
MKUU wa Wilaya  ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti amewataka Wananchi Wa Wilaya ya Buhigwe kuzingatia kanuni za ujenzi kwa kujenga Nyumba zenye ubora na kupanda miti katika Nyumba zao ilikuepukana na majanga yatokanayo na Upepo mkali pamoja na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa .

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Mnyegera ambapo upepo mkali ulitokea huko na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13  wakati akitembelea kuangalia uharibifu huo Gaguti alisema  nyumba nyingi zilizo ezuliwa hazijajengwa kwa kuzingatia kanuni za  ujenzi.

Gaguti alisema ilikuhakikisha tatizo hilo linakwisha Wilaya imeandaa utaratibu wa kupanda miti milioni moja na laki moja  kwa Wilaya nzima na wananchi wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu huo na viongozi wa vijiji wanatakiwa kuzingatia zoezi hilo kila nyumba kupanda miti ya kutosha ilikuepukana na madhara ya kuharibikiwa Nyumba.

Aidha Gaguti aliwaomba viongozi wa kijiji kuwasaidia wote waliopatwa na majanga hayo kwa kipindi hiki ambacho serikali inatafuta namna ya kuwasaidia iliwaweze kupata mahali pa kuzihifadhi familia zao.

"Poleni sana kwa majanga yaliyo wapata nimetembelea kote  ambapo kimbunga kimeezua nyumba lakini hakuna majanga yaliyo tokea ya watu kupoteza maisha wala uharibifu wa mazao ni jambo la kumshukuru mungu kunabaadhi ya Bati zinaweza kutumika nahisi tasmini iliyofanyika  inaweza kupungua,  niwaombe tupande miti ilikujikinga na tatizo hili wakati tunasikitika kwa tukio lililojitokeza na niwaombe viongozi nione jitihada zenu kwa kuwasaidia sisi tutawasaidia kama Wilaya baada ya kuona juhudi zenu za kusaidiana",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mnyegera  Alfonce Ntatie alisema tukio hilo lilitoea mnamo  tarehe 6January ambapo kulitokea upepo mkubwa ambao ulieezua nyumba tisa na Kusababisha uharibifu wa shilingi milioni 13 ambapo Mpaka sasa juhudi za kuwasaidia wathilika wa tukio hilo zinaendelea kufanyika na Wananchi wanaendelea kuwachangia wenzao.

kwa upande wao Baadhi ya Wananchi walio haribiwa nyumba zao na upepo mkari walisema Mpaka sasa wanalazimika kulala nje na familia zao suala ambalo linawapa wakati mgumu hasa ukuzingatia wakati huu ni wakqti wa Mvua.zinaendelea kunyesha na zikinyesha wanalazimika kunyeshewa na watoto wao.
Posted by MROKI On Sunday, January 15, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo