Nafasi Ya Matangazo

January 15, 2017

 Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde leo amekamilisha ziara yake mkoani Mbeya kwa kuwatembelea Vikundi vya Vijana vilivyopo Makongolosi,Wilaya ya Chunya vilivyokopeshwa fedha shilingi 24,000,000 kupitia mfuko wa maendeleo wa Vijana ambapo Naibu Waziri Mavunde aliwapongeza Vijana hao kwa kubuni miradi mbalimbali yenye tija ambayo itawasaidia kujiinua kiuchumi na hivyo kujitengenezea kipato.Vikundi vilivyotembelewa ni Kikundi cha Vijana cha THYROID kinachojihusisha na usambazaji wa vifaa vya umeme jua pamoja na Kikundi cha Vijana wa stendi wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini.
 Aidha pia Naibu Waziri alifanya ziara ya ukaguzi katika kampuni ya Sunshine Mining inayofanya shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.Naibu Waziri Mavunde ameitoza kampuni hiyo  faini ya Tsh 14m kwa ukiukwaji wa sheria ya Afya na Usalama mahali pa Kazi na pia kuamuru wafanyakazi walipwe mshahara kulingana na kima cha chini cha sekta ya Madini ambao awali walikuwa wakilipwa mishahara pungufu.
 Akiendelea na ziara yake...
Wakati huo huo Naibu Waziri Mavunde amemuagiza OCD wa Chunya kuwakamata mara moja raia 10 wa China wafanyakazi wa Kampuni hiyo kwa kutokuwa na vibali vya kufanyia kazi na kuwataka kuwasalimisha katika mamlaka ya Uhamiaji ili waondolewe nchini mara moja kwa kukosa vibali vya ukaazi na vibali vya kufanya Kazi kwa mujibu wa Sheria za Nchi
Posted by MROKI On Sunday, January 15, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo