Nafasi Ya Matangazo

December 07, 2016

Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekari 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga
  Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Ndauka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mradi huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Vibarua akifyaka vichaka kusafisha shamba hilo
 Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) wakisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Samy  Mohammed Elazeb akisimamia maandalizi ya shamba hilo
 Ndauka na Samy  Mohammed Elazeb wakijadiliana jambo
 Mratibu wa Mradi huo, Peter Ambilikile (kushoto) akifafanua jambo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.
 Samy  Mohammed Elazeb (kushoto),  na mwanakijiji wakiziba maji kwenye mabomba ya kisima kilitolewa msaada na taasisi hiyo kwa Kijiji cha Chumbi C


 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chumbi C, akikinga maji kwa mkono katika kisima hicho
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko, akionesha ukumbi wa Kijiji ambao umejengwa kwa msaada wa Taasisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akionesha jengo la ofisi za kijiji hicho, lililojengwa kwa msaada wa taasisi hiyo.
 Nyumba anayoishi Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho
Source: Kamanda wa Matkuio Blog-Richard Mwaikenda.
Posted by MROKI On Wednesday, December 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo