Nafasi Ya Matangazo

November 30, 2016

 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Prof. Ayoub Magimba na Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo  Peter Kisenge.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia Taasisi hiyo. Kulia kwa Balozi ni  Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.
 Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo  Tulizo Shemu Sanga.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo  Peter Kisenge.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait mara baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya katika Taasisi hiyo. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Posted by MROKI On Wednesday, November 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo