Nafasi Ya Matangazo

October 30, 2016

Mitambo ya Kiwanda hicho ambacho huenda kikafungwa kwa kukosa malighafi na kupelekea wafanyakazi wake ambao asilimia kubwa ni wanawake zaidi ya 225 kukosa ajira.
Makamu was Rais, Mama Samia Suluhu alipokuwa na ziara mkoani Mtwara pia aliweza kutembelea kiwanda hicho.
Uongozi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Amama (Amama Farms)kilichopo wilayani Tandahimba mkoani Mtwara umesema kuwa una mpango wa kufunga kiwanda hicho kutokana na kukosa malighafi (korosho).

Akizungumza na waandishi wa habari  meneja wa kiwanda hicho,Abdulrahman Sinani alisema kuwa upatikanaji wa korosho umekuwa mgumu kutokana na kuzuiwa na halmashauri kununua na kutakiwa kwenda kwenye minada.

Alisema kuwa kipindi cha nyuma walikuwa wakinunua korosho kwa kuingia mkataba na vyama vyama vya msingi vya ushirika  (Amcos )na kulipa bei dira inayotangazwa na serikali kwa kuwaongezea wakulima Sh 50 wakati wakisubiri gawio  (bonus).

"Upatikanaji wa korosho umekuwa mgumu kwasababu awali tulikuwa tunaingia mkataba na Amcos kupitia bei dira iliyopangwa na kuongeza Sh 50 wakati tukisubiri bonus,"alisema Sinani na kuongeza

"Suala hili limewahi kutokea na sasa hivi limejitokeza tena kwahiyo mmiliki anaona ni bora kiwanda kifungwe kwasababu makubaliano yaliyokuwepo awali yamesitishwa,"alisema Sinani

Akizungumza suala hilo mkuu wa wilaya ya Tandahimba,Sebastian Waryuba alisema uongozi wa kiwanda hicho tayari ulishaandika barua kwenda kwa waziri mkuu hivyo wanasubiria maamuzi kutoka juu.

Wakizungumza wafanyakazi wa kiwanda hicho walisema kuwa kama kikifungwa kitawaathiri kiuchumi kwani wanakitegemea kuendeshea maisha yao.

Amina Ismail alisema " Wengi tunategemea kiwanda hiki, Mtwara kilikuwepo kiwanda cha Olam nacho kikafungwa tukahamia huku sasa hiki nacho kikifungwa tutaathirika sana, "alisema Ismail

Naye Mussa Bakari alisema "Tunamwomba mmiliki aache nia ya kukifunga kiwanda na badala yake wakutane na uongozi kuona ni kwa namna gani wanapata mzigo kwani sasa hivi tuna mwezi mmoja na nusu hatujafanya kazi, "alisema Bakari

Kiwanda hicho kina wafanyakazi 239 wengi wao wakiwa ni wanawake.

Msimu mpya wa korosho kwa mwaka 2016/17 ulifunguliwa rasmi Septemba mosi mwaka huu na bei dira kutangazwa kuwa ni Sh 1,300 kwa kilo moja ya kirosho ghafi daraja la kwanza na Sh 1,040 kwa daraja la pili   lakini baada ya kufunguliwa minada Oktoba 14 mwaka huu kilo moja imefikia kuuzwa kwa Sh 3,810 bei ya juu ya chini ikiwa Sh 3,700.
Posted by MROKI On Sunday, October 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo