Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2016

 Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
 Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni  mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
 Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
 Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo. 
 Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.

 Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI
 Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na Jackline Kimambo.

Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.

 Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
 Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.

Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni  2016 imemtangaza Diana Edward  kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift  Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
Posted by MROKI On Saturday, September 03, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo