Nafasi Ya Matangazo

June 21, 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Nishati na Madini inawajulisha wananchi wote kuwa siku ya JUMATANO TAREHE 22 JUNI mwaka huu, itatoa huduma maalum ya kukutana na wananchi na kupokea malalamiko, hoja na maoni mbalimbali kuhusu sekta za NISHATI na MADINI.

Huduma hiyo itatolewa na Wataalam wa Wizara sehemu ya mbele ya Jengo la Wizara lililopo POSTA MPYA Mtaa wa Samora, karibu na Jengo la KITEGA UCHUMI.

MUDA ni kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri.

Huduma hiyo maalum itatolewa kama sehemu ya maadhimisho ya WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ambayo huadhimishwa kila mwaka barani Afrika.

Njoo utoe MAONI na KERO yako kuhusu UMEME, GESI, MAFUTA, MADINI na mengineyo kuhusu nishati na madini.

Kwa wale ambao wangependa kuwasilisha kwa njia ya simu na barua pepe, watume kupitia ps@mem.go.tz au caroline.musika@mem.go.tz au simu namba 022 2111749.

WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA

Imetolewa na:                  KATIBU MKUU

                        WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Posted by MROKI On Tuesday, June 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo