Nafasi Ya Matangazo

June 21, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

TSN ni wachapaji w magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spoti leo. Pia ni wamiliki wa kiwanda cha uchapaji cha Standard Printer. 
Posted by MROKI On Tuesday, June 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo