Nafasi Ya Matangazo

June 30, 2016

 Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato M. Mssanzya – CP
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais alikuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo hilo la uhakiki wa silaha
***********
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.

Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha ambazo hazijahikikiwa.  Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo  kupoteza sifa ya kuwa mmiliki halali wa silaha hiyo.

Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.

  Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo

Makao Makuu ya Polisi
Posted by MROKI On Thursday, June 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo