Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2016

Ni kile anacho kitoa mwenye uwezo katika mali yake kwa namna maalum katika usiku wa kuamkia idi au asubuhi ya siku ya idi.

HUKUMU YAKE
Ni fardhi kwa kauli ya Kongamano la Wanawazuoni. 

Dalili
Ibn Omar M/Mungu amuwie radhi kasema

"Kafaradhisha Mtume wa Allah S.A.W Zakaa ya Fitri ya kumaliza Ramadhani pishi moja ya tende, au pishi moja ya ngano, kwa mtumwa na aliye huru, na mwanamme na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika Waislamu"

Na Pia kuna kauli inayosema kuwa ni sunna iliyohimizwa.

FADHILA YA ZAKKATUL FITRI

Mwenyezi Mungu katika Suratil Aalaa, aya 14-15

قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّىٰ...وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ.
Hakika amefanikiwa aliyejitakasa...Na akalitaja jina la Mola wake na akasali.

Wamesema baadhi ya wanazuoni Watafsri kwamba kujitakasa kunako kusudiwa hapa ni kutoa Zakaa ya Fitri, na kwamba sala hapa ni sala ya Idi.

Imepokewa kwa Ibnu Abbas R.A kasema

"Kafaradhisha Mtume (S.A.W) zakaa ya Fitri ili kumtakasa mwenye kufunga na kosa la kusema upuuzi na machafu, na ili kuwalisha maskini"

Kupitia kutoa Zakatul fitri kunapatikana kuwalisha maskini na kuwaondolea shida zao hasa katika siku ya idi.

ambayo ni siku ya furaha kwa Waislamu wote.

Mtume S.A.W Anasema ;

"Watoshelezeni katika siki hii" BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

KIWANGO KINACHOTOLEWA.
Hutolewa kwa kila mtu pishi moja ya chakula kama ilivyokuja katika hadithi. Na inavyotakiwa ni kutoa chakula chenyewe, kwani ndivyo hadithi zilivyoeleza, ingawa kuna Wanawazuoni wametoa ruhsa ya kutoa thamani ya chakula kinachotolewa, ambapo kiwango cha pesa kinachotolewa huwa sawa na thamani ya pishi moja ya chakula. 

Pishi ya mchele inakadiriwa kwa kilo mbili na gramu hamsini (2.05kg)

WAKATI WA KUTOA ZAKATUL FITRI

Wakati bora wa kutoa Zakatul Fitri ni asubuhi ya siku ya Idil-Fitri kabla ya Sala ya Idi. Na inajuzu kuitoa usiku wa kuamkia Idi .

"Atakaeitoa kabla ya Sala huwa ni zakaa iliyokubalika, na atakaeitoa baada ya Sala, huwa ni moja katika Sadaka"_

Kwa hiyo haitakikani icheleweshwe mpaka Sala ya Idi ipite, lakini asiyewahi kuitoa wakati huo anatakiwa aitoe hata baada ya hapo.

N.B 

Kwa Maelezo yaliyopita baada ya kutekeleza PROGRAMU YETU KWA UZURI YA MFUTURISHE NDUGU YAKO KWA TENDE AU MAJI. 

Tunaileta kwenu Programu hii ya Zakatul fitri kwenu . MFURAHISHE NDUGU YAKO MUISLAMU  SIKU YA EID NA MTOE UNYONGE WA KUOMBA OMBA SIKU HIYO YA FURAHA KWA WOTE.

Kwa More updates , wafatilie  facebook :- Kijana wa Kiislam Dsm.

JIUNGE KUPITIA NAMBA.
0715800772,0673800772,0689604780.
Na Mratibu , Msimamizi GHALIB N MONERO.
Posted by MROKI On Tuesday, June 28, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo