Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2016

KATIKA kuhakikisha  madereva wanaosambaza bidhaa za kampuni wanafanya kazi zao kwa ufanisi,kampuni ya TBL Group imeandaa mafunzo maalumu kwa madereva kutoka viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Moshi,Mbeya na Mwanza.

Mafunzo hao ambayo yamemalizikia mkoani Arusha yaliendeshwa na mkufunzi wa madereva kutoka kampuni ya CFAO Motors,Hubert Kubo (pichani juu) ambaye amewapatia madereva hao elimu  ya udereva wa kujihami ikiwemo utunzaji wa vifaa wanavyoviendesha.

Baadhi ya madereva waliohudhuria mafunzo hayo walishukuru mwajiri wao kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali kuhusiana na kazi yao ambayo walidai yanawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi na kuwa na  uwezo wa kukabili changamoto mbalimbali za kikazi kwa urahisi.
 Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha.
Mkufunzi wa madereva kutoka kampuni ya CFAO Motors,Hubert Kubo akiendelea na mafunzo hayo. 
 Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha.
Posted by MROKI On Monday, June 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo