Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2016

Mwanamke kutoka Tanzania Lilian Makoi Rabi amekuwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya ubunifu wa kuleta mabadiliko kwenye jamii inayotolewa na Kongamano la Uchumi Duniani linalofanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu limefanyika mjini Kigali nchini Rwanda.
 
Shindano la kuwania tuzo hiyo linahusisha taasisi na kampuni ndogondogo zinazotoa huduma mbalimbali za ubunifu wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii katika sekta mbalimbali.
 
Lilian  kutoka taasisis ya bimaAFYA ametunukiwa tuzo kutokana na ubunifu wake katika kuboresha huduma za bima ya afya nchini kwa kuweka mfumo usio na urasimu wa kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini na wasio na ajira katika sekta rasmi kuweza kujiunga na mfumo wa bima ya afya na kupata matibabu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo huduma hiyo iliwafikia waajiriwa waliopo kwenye sekta rasmi pekee.
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kongamano la Uchumi duniani imeeleza kuwa ubunifu huu umeonekana unaweza kusaidia kuboresha huduma za bima za afya katika nchi mbalimbali za Afrika na kuanzia sasa mpaka mwaka ujao huduma za bimaAFYA zitaanza kutolewa katika nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Nigeria na Ghana.
 
Washindi wengine wa tuzo hii  ya ubunifu  wenye kuleta mabadiliko ni Natalie Bitature (Uganda),Audrey Cheng (Kenya),Nneile Nkholise (Afrika ya Kusini),Larissa Uwase (Rwanda)
 
Taarifa ya Kongamano hili imeeleza kuwa mabadiliko ya Afrika yataletwa na vijana ambao ndio wenye idadi kubwa ya  watu wanaoishi barani Afrika na ndio maana imeanzisha shindano la kuyaenzi makampuni yanayofanya kazi  kwenye nchi mbalimbali za Afrika yakiwa yanatoa huduma zenye ubunifu wenye kuleta mabadiliko na kuwa inafurahisha kuona wanawake wajasiriamali hawajaachwa nyuma katika kuanzisha taasisi na kampuni zenye huduma za kuleta mabadiliko.
 
“Karne ya 21  itakuwa karne ya Afrika,hivyo vijana popote walipo wanapaswa kuamka na kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kulifanya bara la Afrika kusimama  na kujitegemea katika Nyanja mbalimbali”.Alisema Elsie Kanza,Mkuu wa kongamano hilo katika ukanda wa bara la Afrika.
 

Washindi wote wa tuzo  na washiriki wa shindano hilo waliofanya vizuri walialikwa kwenye Kongamano la Uchumi Duniani nchini Rwanda lililokuwa na washiriki Zaidi ya 1,200,000 kutoka nchi Zaidi ya 70 duniani ambapo walipata fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao pia
Posted by MROKI On Sunday, May 15, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo