Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2016

Bundala Alex Semamba akiwa na  Mkurugenzi wa SABMiller wa kanda ya Afrika,Mark Bowman na wafanyakazi  wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati wa hafla ya kutumiwa tuzo
  Bundala Alex Semamba akiwa wafanyakazi  wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati wa hafla ya kutumiwa tuzo
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya konyagi Bundala Alex Samamba ametunikiwa tuzo kubwa inayojulikana kama SABMiller Africa Master,tuzo inayotolewa kwa wafanyakazi wa muda mrefu na waliotoa mchango wa pekee kuendeleza kampuni na ni moja ya tuzo kubwa na inayoheshimika kwa kampuni hiyo.

Hafla ya kutunukiwa tuzo hiyo ilifanyika katika mkutano maalumu wa maafisa mauzo na masoko wa kampuni ya SABMiller uliofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini wiki iliyopita na alitunikiwa tuzo hiyo na Mkurugenzi wa SABMiller wa kanda ya Afrika,Mark Bowman akiwa ni mtanzania peke yake na mfanyakazi wa kwanza wa kampuni ya Konyagi  kuipata.

Akiongea muda mfupi baada ya kupata tuzo hiyo Bundala alisema kuwa anawashukuru wafanyakazi wenzake wote ambao akifanya kazi nao kwa ushirikiano kwa kuwa mafanikio mara  nyingi yanapatikana kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano.

“Tuzo hii japo nimetunukiwa mimi lakini ni kwa ajili ya wafanyakazi wote wa kampuni ya Konyagi ambao nimekuwa nikifanya nao kazi kila siku na kukabiliana a changamoto mbalimbali za ushindani zilizopo katika masoko kwa sasa”.Alisema

Anakumbuka safari mbalimbali alizopitia katika kazi za mauzo ambazo anaeleza kuwa zinahitaji kuwa mtu mwenye bidii ya kazi na kufanyika  kazi ushauri wa wateja “Pamoja na elimu na nyadhifa nilizoshikilia nilipokuwa kwenye  kazi za usambazaji nilikuwa nafanya kazi pia ya udereva wa malori makubwa ya kufikisha bidhaa kwa wateja na wakati mwingine kulazimika  kupakua mzigo”.Anasema Alex.

Bundala alijiunga na kampuni ya Konyagi miaka 22 iliyopita katika Idara ya mauzo na Masoko na kutokana na bidi katika kazi aliweza kupandishwa cheo kuwa Meneja Masoko na Mauzo anayesimamia kanda mbalimbali.


Kutokana na umahiri wake katika ubunifu wa mauzo na uendelezaji wa masoko alipandishwa Cheo kuwa Meneja wa kuendeleza Masoko wa kampuni ambapo baadaye aliteuliwa kushika nafasi aliyonayo kwa sasa hivi ya Meneja Uendeshaji wa kampuni.
Posted by MROKI On Sunday, May 22, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo