Nafasi Ya Matangazo

April 19, 2016


Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mch Petter Msigwa akimpongeza mbunge wa viti maalum RithaKabati mara baada ya kuapishwa sambamba na watu wengi walimpongeza mbunge huyo kama wanavyoonekana kwenye picha.

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo mkoani iringaVennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa.

 watu mbalimbali walijitokeza kumpongeza mbunge Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa hii leo.


 mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo mkoani iringaVennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum rita kabati mara baada ya kuapishwa.

na fredy mgunda iringa. 
mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritha Kabati ameapishwa leo kuwa mbunge kamili hii imekutaja mara Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane (8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatangaza ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu  
Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.

hata hivyo mbunge wa iringa mjini mchungaji petter saimoni msingwa na mbunge wa jimbo la kilolo vennance mwamoto ambaye nia ndugu na ritta kabati kwa pamoja walimpongeza kwa kuchaguliwa  na kuapishwa kwake siku ya leo.
Posted by MROKI On Tuesday, April 19, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo