Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2016

Meneja   wa biashara wa kampuni ya  simu za mkononi nchini  Airtel  kanda ya nyanda  za  juu  Bw Straton Mushi (kushoto) akimkabidhi  jana kaimu  mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bw  Richard Kasesela msaada  wa saruji mifuko 100 na mabati  200 vyenye  thamani ya Tsh milioni  5  kwa ajili ya kusaidia waathirika  wa mafuriko Pawaga  na Idodi wilaya ya   Iringa.
Kaimu  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Bw Richard Kasesela (kulia ) akipokea  msaada wa bati 200 pamoja na  saruji  100  vyote  vikiwa na thamani ya  Tsh milioni 5 kutoka kwa meneja  wa biashara  wa Airtel kanda ya nyanda za juu Bw Straton  Mushi jana   msaaada   uliotolewa kwa ajili ya  waathirika  wa mafuriko Pawaga na Idodi  wilaya ya Iringa.
 Kaimu  mkuu  wa mkoa wa Iringa Bw  Richard Kasesela (kushoto mwenye suti)  akimpomngeza meneja  wa biashara  wa Airtel kanda ya nyanda za juu Bw Straton Mushi kwa niaba ya kampuni hiyo  simu  za mikononi kwa  kusaidia waathirika wa mafuriko Pawaga  na Idodi  Iringa.
*****************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika jimbo la Isimani, wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu kwaajili ya ujenzi wa makazi baada ya makazi yao ya awali kuzoewa na mafuriko. Zaidi ya familia 220 zimepoteza makazi kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa Februari mwaka huu.

Akiongea wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel kanda ya Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizoathirika na mafuriko haya.

Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao ya chakula na biashra kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja na wakazi wa Iringa vijijini ili kuwawezesha kujenga makazi yao upya. Leo kwa niaba ya Airtel kupitia ofisi yetu ya kanda ya juu kusini tunatoa msaada wa mabati 200 na saruji mifuko 100 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa Isimani ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee. Pia huu ni wakati muhimu wa kushirikiana  kuwawezesha wenzetu kurudi na kukaa na familia zao ili kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Isimani, Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu umekuja wakati tunauhitaji zaidi, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchangia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.
Posted by MROKI On Wednesday, March 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo