Nafasi Ya Matangazo

December 01, 2015

 Basi la Taqbir namba T 230 BRJ likiwa eneo la tukio.


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Tabora zinaarifu kua basi la Taqbir namba za usajili T 230 BRJ lililokua likitokea jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Geita limepata ajali majira ya saa 2 usiku maeneo ya Shelui Wilaya ya Iramba mkoani Singida katika barabara kuu ya Singida-Tabora kuelekea Igunga. 

Shuhuda wetu anasema ajali hiyo imesababisha vifo na majeruhi kadhaa baada ya kugongana na Lori la mafuta na kuharibika vibaya.

Hadi muda huu abiria wa mabasi mengine ndo wanaendelea na wokozi.
Father Kidevu Blog itawaletea habari kamili hapo baadae.
Posted by MROKI On Tuesday, December 01, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo