Nafasi Ya Matangazo

July 24, 2015

Huku usalama ukiwazuia maelfu ya mashabiki wa rais wa Marekani kukutana naye ama hata kuhudhuria kongamano atakalohutubia katika ziara yake ya siku tatu mjini Nairobi Kenya, kundi la waimbaji kutoka jamii ya kimaasai imepata fursa ya kipekee.

Waimbaji hao wametunukiwa jukumu la kumtumbuiza rais Obama. Kundi hilo la Olalang ndilo litakalomburudisha rais Obama atakapozuru Kenya leo. Kundi hilo la Kimaasai kutoka mji wa Maasai Mara nchini Kenya limeandaa nyimbo na densi za kimaasai tayari kabisa kukonga moyo wa kiongozi mwenye nguvu zaidi duniani. 

Kundi hilo linalowajumuisha wanaume na wanawake kutoka jamii ya maasai limekuwa likifanya mazoezi kwa zaidi ya miezi mitatu tangu lilipoarifiwa kuwa litamtumbuiza rais Obama. Soma zaidi BBC
Posted by MROKI On Friday, July 24, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo