Nafasi Ya Matangazo

July 08, 2015

AfisaMasokonaUtafiti, Andes Seiyaakiwaelezeawadauwaliotembeleabanda la AICC hudumazinazotolewana AICC katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu sabasaba..

MwenyekitiwaBodiya AICC, Balozi Christopher C. Liundiakisainikitabu cha wagenialipotembeleabanda la AICC, katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu sabasaba.



Mwenyekiti wa Bodi ya AICC akibadilishana mawasiliano na mmoja wa wadau kutoka China alipotembelea banda la AICC katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu sabasaba.

**********
KITUO cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kimeshiriki maonesho ya 39 ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ili kuelezea umma juu ya shughuli zake mbalimbali ikiwemo masuala ya uendeshaji wa mikutano.

AICC ilielezea pia uwepo wa kituo chake cha Mikutano kwa Mkoa wa Dar es Salaam kijulikanacho kama Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) chenye kumbi zenye uwezo wa kuhudumia wageni 10-1000.

Mbali na masuala ya mikutano AICC pia iliweza kuwaelezea wadau mbalimbali walio tembelea banda lao juu ya huduma ya upangishaji wa nyumba za kisasa za makazizilizopo eneo la Fire na Range Road jijini Arusha na uwepo wa nafasi za kupanga kwa ajili ya Ofisi kwenye Makao Makuu ya AICC jijini Arusha.
Posted by MROKI On Wednesday, July 08, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo