Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2015

 
MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Marehemu Eugin Elishiringa Mwaiposa  (55) anataraji kuzikwa kesho Juni 6,2015 nyumbani kwake Kipunguni B.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia waliambia Father Kidevu Blog kuwa, Mwili wa marehemu uliwasili juzi na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na mazishi yanasubiri watoto wa marehemu walioko nje ya nchi.

Leo Ijumaa mwili wa Marehemu utapelekwa nyumbani kwake na utalala hapo hadi kesho wakati wa mazishi.

Wistone Simbo amesema watoto wa marehemu wanaosubiriwa ni Mecktilda aliyeko nchini Canada na Samira aliyeko masomoni nchini Malaysia. 

Aidha Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano leo walitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Mbunge huyo katika ibada iliyoendeshwa viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kuhudhuriwa na mume wa marehemu  Ally Ibrahim Mwaiposa, Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi,a Naibu Spika wa Bunge na mawaziri.

Vilio na huzini vilitanda katika viwanja vya Bunge wakati watumishi wa Bunge, Wabunge, Mawaziri na wanahabari wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu hii leo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

 Akizungumzia msiba huo kwa kunukuu mtari wa Biblia wa Ayubu 14:1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi”, Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni diwani wa Gongo la Mboto, Jerry Silaa amesema ni pigo kubwa kwa jimbo la Ukonga na Halmashauri yake ya Ilala ambayo marehemu alikuwa ni Diwani hasa kutokana na kifo hicho kuwa cha ghafla.

“Hakika Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, Mwaiposa ni bora angekuwa aliumwa tukamuuguza lakini kifo hichi ni cha ghafla sana na hatuna budi kushikamana sote bila kujali itikadi zetu za kisiasa na tumzike ndugu yetu,” alisema Silaa.

Nae Diwani wa Kata ya Kipawa, jimbo la Segerea, Bona Kaluwa amesema sema kifo cha Mbunge wa Ukonga, ni pigo kwake na jamii nzima kwani alikuwa ni mtu wake wa karibu na majirani ambapo alikuwa ni mshauri wake mkuu wa masuala mbali ya kisiasa na familia kwa ujumla.

  
Mume wa Marehemu,  Ally Ibrahim Mwaiposa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mkewe Eugen Mwaiposa katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
 Waombolezaji wakiwa viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Friday, June 05, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo