Nafasi Ya Matangazo

May 09, 2015

 Mtemvu akiitembelea Nyumba ya Bi Mwashamba Mwandoro maeneo ya Kurasini,  baada ya ukuta wa Nyumba kuanguka kutokana na Mvua zinazo endelea kunyesha Dar es Salaam na hapo akiongea akiwa katika nyumba hiyo, katika msafara huo aliongozana na Meya na Naibu Meya wa Temeke ,na Diwani wa maeneo hayo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Abdon Kidege, akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa ziara ya kutembelea na kuwaona wananchi waliopatwa na mafuriko ya Mvua zinazo endelea kunyesha
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi walio patwa na mafuriko maeneo ya Wailesi alipo watembelea
 Madereva wa Magari ya Abiria yanayo fanya safari kati ya Tandika - Yombo Kilakala kupitia Daraja la Tazara na Tandika kwa Limboa wakishirikiana kujaza viroba vya mchanga na kuweka sehemu yamaeneo ya  Barabara hiyo ili waweze kupita kwa urahisi     
 Madereva hao wakiwa wanapakia mchanga kwa kuweka katika maeneo nkorofi ambayo yanasababishwa.
 Magari yakipita kwa shida na eneo hilo linauterezi kitu ambacho ni hatari sana kwa wanao tumia njia hiyo
 Magari mengine yalazimika kushushia katikati ya Daraja kitu ambacho ni hatari na wengine kupata nafasi ya kuosha Pikipiki zao

 Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji
  Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji
 Mbunge Mtemvu akiyapima maji kwa kuingia na kujionea
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yombo Relini Yusufu Marko (kulia) akimwelekeza jambo wakati alipo fika katika maeneo hayo baada ya kuzunguuka maeneo tofauti na  Mbunge Abbas Mtemvu (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Posted by MROKI On Saturday, May 09, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo