Nafasi Ya Matangazo

May 05, 2015

Kufuatia mgomo wa madereva wa magari ya abiria ulioanza tarehe 04/05/2015, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP D.A.MISIME amesema, “ watu 37 wamekamatwa katika mitaa ya Nkuhungu na Chadulu Manispaa ya Dodoma baada ya kufanya fujo barabarani kuzuia watu wengine kutoa huduma ya usafiri kama Bajaji na magari ya watu binafsi kwa kuwapiga watu wanaopanda vyombo hivyo vya usafiri, kupiga magari kwa mawe na kufunga barabara”.

Akifafanua kuhusu kukamatwa kwa watu hao 37 amesema ni wale tu waliokwenda mbali zaidi na kujichukulia sheria mikononi, wale wote walioegesha magari yao kwenye vituo au pembezoni mwa barabara hawakukamatwa. 

Kamanda MISIME ametoa wito kwa watu wote kwamba ni marufuku watu kuzuia wengine kutoa huduma, ni marufuku watu kuharibu mali za wengine. Wanaofanya uharifu huo watakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. 
Posted by MROKI On Tuesday, May 05, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo