Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2015

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma. SACP David Misime
WATU wanne wamepoteza maisha jana Aprili 10 mwaka huu badaa ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Nyahunge  lenye namba za usajili 506 CSX Youtong kugongana uso kwa uso na gari  lenye namba za usajili T. 856 ALM Toyota Mark II katika eneo la Nzuguni barabara kuu ya Morogoro Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, SACP David Misime amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali ni dereva wa gari dogo aliyeingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari.

Kamanda Misime amewataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.      JACKSON LAZARO, mwenye miaka 51, Askari wa JWTZ Monduli Arusha na Mkazi wa Nzuguni aliyekuwa akiendesha gari dogo.
2.      HELENA  MICHAEL CHIUYO, miaka 36  na mkazi wa Makole.
3.      FATUMA PATRICK MTAUGA, miaka 17, Mwanafunzi Kidato cha Tatu City Sekondari  na mkazi wa Makole.
4.      STELLA BATON GIDEONI, mwenye miaka 35 mkazi wa Kisasa. 

 Ajali hiyo ilitokea katika makutano ya barabara inayotokea Kijijini Nzuguni, ambapo dereva wa gari ndogo alikuwa akitokea kijijini Nzuguni kuingia barabara kuu ya Dodoma/ Morogoro na kugongana na Bus ambalo lilipoteza mwelekeo na kuingia porini umbali usiopungua mita 300 na kugonga mti kisha kusimama. Katika Bus majeruhi wawili walipata michubuko kiasi na walitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa. 

 Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari ndogo T. 856 ALM Toyota Mark II kuingia barabara kuu bila kuwa makini na kusababisha kushindwa kumpa kipaumbele aliyekuwa barabara kuu kupita  kwanza lakini pia  mwendo kasi wa dereva wa bus kumesababisha madhara kuwa makubwa. 

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ametoa wito kwa madereva pamoja na wanaosomea udereva, kufuata sheria za usalaba barabarani, wanapaswa kila mara kuzingatia udereva wa kujihami kwamba ninapoendesha gari linaweza kutokea jambo lolote lile mfano dereva mwenzangu kukosea, mtembea kwa miguu kukatisha ghafla nk. 

Je, kwa mwendo huu nitaweza kusimama bila kuleta madhara? Hata kama nikishindwa madhara yasiwe makubwa, busara na kutokulipiza kisasi.
Posted by MROKI On Saturday, April 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo