Nafasi Ya Matangazo

April 27, 2015

 Balozi wa Tanzania nchini China, Mh Abdulrahman Shimbo akitoa mawaidha kwa waalikwa katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilziofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB).(
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa tatu kushoto) na mkewe Mama Shimbo (wan ne kushoto), wakiwa na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB) katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi.
 Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa pili kushoto) na mkewe (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Wanafunzi Beijing kutoka nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi.
Wanafunzi Wakitanzania Beijing pamoja na wageni mbalimbali katika picha yapamoja na mgeni rasmi, Balozi wa Tanzania nchini China, Abdurahman Shimbo (mwenye suti katikati) na mkewe, katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa  Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Beijing  (TZ-SUB) na kufanyika Ubalozini mjini hapa.
Balozi wa Tanzania, China, Mh Abdulrahman Shimbo (wa nne kushoto) na mkewe Mama Shimbo (wa tano kushoto)katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa  Wanafunzi Watanzania kutoka vyuo mbalimbali mjini Beijing katika sherehe za  miaka 51 ya Muungano Ubalozini. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB), Ireneus Kagashe (kulia) akitoa utangulizi katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi wa sherehe hizo, Balozi wa Tanzania, China, Mh. Abdulrahman Shimbo, Mkewe Mama Shimbo na Katibu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi nchini China, Michael.
Familia na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Sherehe hizo ziliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB). Wa sita kutoka kushoto ni mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo, kushoto kwake ni mkewe, Mama Shimbo
***********

Na Mwandishi wetu, Beijing
WATANZANIA wametakiwa kuliombea Taifa amani na kuulinda Muungano kwa kuwa ndio njia pekee inayowaunganisha wananchi na hata kujenga undugu kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mwito huo ulitolewa na Balozi wa Tanzania nchini hapa, Abdulrahman Shimbo, katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliopelekea kuzaliwa Tanzania. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB), zilifanyika Ubalozini, mjini hapa.

Balozi Shimbo alisema waasisi wa Muunganio, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume waliasisi suala hilo kwa kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili na lengo likiwa kuiunganisha Afrika Mashariki.

Alisema Muungano umezalisha nchi ya Tanzania ambayo pamoja na mambo mengi mema yaliopo, pia nchi nyingi duniani ikiwamo China zimejipanga kuwekeza katika uchumi wa viwanda ambao kwa muda mrefu umekuwa ukisuasua.

Katika hatua nyingine, Balozi Shimbo aliwataka wananchi kutumia ardhi kama njia pekee ya kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya, kwa kuitumia kuwekeza na kuwaajiri vijana ili kulilinda Taifa dhidi ya kuangamia kwa nguvu kazi yake yaani vijana.

Balozi alisema ardhi iliyopo nyumbani Tanzania, inatosha kuleta mapinduzi ya ajira kwa vijana nchini, na kuwataka wananchi kuitumia kwa mujibu wa utaratibu uliopo, kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Mwito huo aliutoa kufuatia igizo lililofanywa na TZ-SUB likibeba ujumbe wa “Tuungane kutokomeza dawa za kulevya” ukienda sambamba na matukio ya kukamatwa kwa watanzania nchini China, wengi wakiwa vijana wakijihusisha na biashara ya kusafirisha dawa hizo.

 “Igizo ni ujumbe tosha, vijana na watu wazima baadhi wanajidanganya kutafuta fedha isiyo halali, biashara hii ni ya dhambi na inaharibu vizazi, vijana wengi hawawezi kutibiwa tena, fedha za dhambi zinatisha,” alisisitiza Balozi Shimbo.

Sherehe hizo zilizoambatana na burudani ya igizo na muziki, zilihudhuriwa pia na viongozi wa Wanafunzi wanaosoma Beijing kutoka nchi za EAC ikiwamo Uganda, Rwanda na Burundi. Wakitoa salamu zao, viongozi hao wa EAC waliisifu Tanzania kwa Muungano na kuomba udumu.
Posted by MROKI On Monday, April 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo