Nafasi Ya Matangazo

March 24, 2015

Mteja wa muda mrefu wa  bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati)  akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths  jijini Dar es Salaam.
 Mteja wa muda mrefu wa  bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati)  akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths  jijini Dar es Salaam.
**********
Na Mwandishi Wetu         
Katika pindi hiki cha sikuu ya Pasaka watanzania wanaweza kununua nguo zenye ubora kwa nusu bei kufuatia punguzo la silimi 50 lililotangazwa jana na duka maarufu la nguo la Woolworths jijnini Dar Es Salaam.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa punguzo hilo, mkurugenzi wa duka hilo Joehans Bushiri aliawambia wateja waliofika dukani hapo kuwa punguzo hilo titadumu kwa muda wa wiki nne.
 
Alisema lengo kubwa la Woolworths ni kuwawezesha watanzania wenye vipato  vya aina mbali mbali kufurahia sikukuu ya Pasaka kwa kupata nguo za kisasa zenye ubora kwa gharama nafuu.
 
Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kuachana na nguo za mtumba“Tunawasihi watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths linatoa punguzo kubwa ili kuwawezesha watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.,” alisema.
 
Bushiri alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa nchini, litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea nguo nzuri na zenye ubora kwa gharama nafuu na hivyo kuwasaidia kuepukana na nguo za mtumba.
 
“Mteja anayekuja kununua nguo dukani kwetu anakuwa amefanya uamuzi sahini kwani atapa nguo zenye ubora kwa gharama nafuu na atakuwa amepata kitu ambacho kinaendana na thamani ya pesa yake,” alieleza
 
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, duka hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo hadi kwa muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutusha kulipa mara moja kuweza kufurahia nguo zenye ubora.
 
Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa mda muafaka, Woolworths imeweza kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa inatumia usafiri wa ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tun kunatumia muda wa mwezi mmoja hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia mda wa wiki mbili hadi tatu.
 
Bwana Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama zinazopatikana South Africa na kwa bei zinazofaa kabisa. 
 
Kwa upande wake Manfred Ngatunga ambaye ni mmoja kati ya wateja wazuri wa duka hilo alitoa shukrani zake kwa uongozi wa duka hilo kwa kutoa punguzo kubwa haswa katika mismu huu wa sikuu ya Pasaka.
 
Uamuzi wa punguzo la bei umekuja kipindi kizuri sana. Kipindi hiki na kipindi ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya sikuu ya Pasaka. Tunashukuru kwa kuwa tutapata nguo zenye ubora kwa nusu bei, kila mtu sasa anaweza kupendeza,” alieleza.
Posted by MROKI On Tuesday, March 24, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo