Nafasi Ya Matangazo

March 27, 2015

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia), akizungumza na viongozi wa ujumbe wa Serikali ya Sudan Kusini waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam jana.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, akizungumza katika kikao cha mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na viongozi wa Sudan Kusini. (wa pili kushoto)  ni Mkurugenzi  wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi Eng. Venny Ndaymukama, anayemfuatia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara za Mkoa Eng. Laurent Kyombo.

Naibu Waziri wa Usafirishaji, Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mh. Simon Mijok, akitoa salamu za Serikali yake kwa viongozi wa Wizara ya ujenzi, kutokana na ziara ya mafunzo ya siku tatu inayoendelea hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Dr. James Wanyancha, akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Usafirishaji, Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mhe. Simon Mijok alipotembelea ofisi za Mfuko wa Barabara kwa ajili ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara jijini Dar es salaam.

Ujumbe wa Sudan Kusini katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) walipoitembelea Bodi hiyo jana kujifunza inavyofanyakazi.
Posted by MROKI On Friday, March 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo