Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2015



Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja na Afisa habari, mwandamizi, Elimu na Mawasiliano, Veneranda Malima. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya hali ya urejeshaji mikopo ya wanafunzi. Kushoto ni Mkurugenzi Urejeshaji wa Mikopo wa HESLB, Juma Chagonja na Afisa habari, mwandamizi, Elimu na Mawasiliano, Veneranda Malima.
*******
IMANI potofu kuwa mikopo itolewayo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),  ni ruzuku na hawapaswi kuirejesha ni moja ya changamoto ambazo bodi hiyo inakabiliana nazo katika ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika.

Wakizungumza katika mutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo maofisa kutoka HESLB wamesema makusanyo yamekuwa yakisua sua kutokana na wakopaji kutofanya marejesho na kukaa kimya hata wanapo andikiwa.

Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, amesema kuwa jumla ya shilingi Bilioni 123.8 zilipaswa kuwa zimerejeshwa lakini hadi sasa bodi imekusanya Bilioni 65.2 pekee.

Bodi ya mikopo imekopesha wanafunzi kiasi cha shilingi Trilioni 1.8 tangu mwaka wa masomo 1994/95 hadi Juni mwaka 2014 kati ya fedha hizo bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.

Mwaisobwa alisema jumla ya wadaiwa 136,198 sawa na asilimia 76.94 ya wadaiwa wote 177,017 ambao mikopo yao imeiva wametambuliwa na wanaendelea na marejesho ya mikopo.
“Hadi sasa mikopo yote inayotolewa na Bodi kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 inabeba tozo la utunzaji wa thamani ya mikopo kwa asilimia sita kwa mwaka kwa kiasi chote cha mkopo ambacho hakijarejeshwa” alisema.
Alisema bodi hiyo inaendelea kuongeza kasi ya urejeshaji wa mikopo kwa kubuni mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kurejesha mikopo na kuongeza matumizi ya mitandao ya simu katika kukusanya madeni.
Aidha njia mbadala za utumiaji wa huduma za kifedha za mitandao ya simu kama M Pesa na Airtel Money nazo zimeanza kutumika ili kuwarahisishia wakopaji namna ya kurejesha fedha hizo badala ya kwenda kupanga folebni benki.

Pia alisema wamezidisha ushirikiano zaidi na wadau muhimu hasa Mifuko ya Hifadhi ya Jamiii, Mamlaka ya Mapato, Waajiri, Sekta isiyo rasmina Wanufaika wa mikopo ambapo pia wamechukua hatua za kisheria dhidi ya wanufaika wanaokaidi kurejesha mikopo yao ambapo hadi sasa kuna kesi 18 zimefunguliwa mahakamani dhidi ya wadaiwa sugu.
Posted by MROKI On Wednesday, March 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo