Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2015

Timu ya Yanga leo imewapaa kileleni mwa ligi baada ya kuwabanjua Prison ya Mbeya katika uwanja wake wa nyumbani wa Sokine kwa mabao 2-1.

Mabao ya yanga yalifungwa na wajuzi wale wale walioibanjua katika mchezo wa awali jijini Dar es Salaam  iliposhinda mabao 2-1.

Magoli ya Yanga yamefungwa katika kipindi cha kwanza na  Simon Msuva aliyepachika wavuni goli la kwanza na la tatu huku Andrey Coutinho akifunga goli la pili. 

Katika mchezo kwanza uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Andrey Coutinho  dakika ya 38, bao la pili lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 69, huku bao la Prisons likifungwa na Ibrahim Kahaka, katika dakika ya 67.
Mlandizi huko nako Azam FC imekubali kugawana pointi na Ruvu Shooting katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mabatini mjini humo baada ya kutoka sare ya 0-0.
Posted by MROKI On Thursday, February 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo