Nafasi Ya Matangazo

January 28, 2015

Mnamo tarehe 26/01/2015 majira ya 15:55hrs katika eneo la Nala kwenye Mzani wa Magari (Weight Bridge) Kata ya Nala Tarafa ya Zuzu Manispaa ya Dodoma walikamatwa watu wanne (4) raia wa Ethiopia wakiwa kwenye basi la Prince Munaa lenye namba za usajili T. 788 CNK likitokea Mwanza Kuelekea Dar es Salaam.

Watu hao ambao ni:-
1.    SULYAN S/O JEYLAN mwenye miaka 23, Mkazi wa Kolobi – Ethiopia.
2.    KIAR S/O TAHIR HUSSEN mwenye miaka 25, Mkazi wa Agerifa – Ethiopia.
3.    BELAYNEH S/O DANIEL LEMENGO mwenye miaka 22, Mkazi wa Durame – Ethiopia.
4.    GALASA S/O AHMED GELIL mwenye miaka 24, Mkazi wa Robe – Ethiopia wakiwa na hati za kusafiria (Passport) zilizogongwa muhuri wa mwisho mpakani mwa Ethiopia na Kenya eneo la Moyale Border tarehe 16/01/2015.

Pia amekamatwa wakala anayehusika na kuwasafirisha watu hao aliyefahamika kwa jina la SULTAN S/O SAID RAMADHANI @ KUSHARUNGA mwenye miaka 31, mkazi wa mtaa wa Mecco Jijini Mwanza ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Kusharunga Tarafa ya Kimani Wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Wahamiaji hao haramu walikuwa wanasafirishwa na wakala wao huyo kuelekea Afrika ya Kusini kupitia Mtwara kuelekea Msumbiji hatimaye kufikia Afrika ya Kusini. Aidha watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
Posted by MROKI On Wednesday, January 28, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo