Nafasi Ya Matangazo

October 02, 2014

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana (Kulia)akisalimiana na Rais wa  Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba  wakati wa  mkutano mkuu wa kwanza wa AATO  unaofanyika Zanzibar   kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Dkt.  James Diu.
 Rais wa  Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba  (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa AATO  Bi Margreth Kyarwenda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) , kinachomilikiwa na TCAA wakati wa  mkutano mkuu wa kwanza wa AATO  unaofanyika Zanzibar   kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
 Baadhi ya wataalamu wa sekta ya  Usafiri wa Anga Tanzania wakifuatilia kwa karibu mkutano  mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Baadhi ya wataalamu wa sekta ya  Usafiri wa Anga toka nchi ya Senegal  wakifuatilia kwa karibu mkutano  mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar  kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana.  J. Mbwana (katikati)   akiwasikilza  wajumbe wa mkutano  wa AATO , baada ya kufungua mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Wengine  kutoka kushoto ni  mjumbe wa Bodi TCAA,  Yussuf . M. Ali, Mkurugenzi  Idara Udhibiti  Uchumi , TCAA, Dkt. James Diu , Rais wa AATO Tchagbele Sadamba  na   Mjumbe wa Bodi TCAA. Hanif.  M. Malik.
Mkurugenzi  Idara ya Udhibiti Uchumi(TCAA) Dkt. James Diu , akitoa hotuba kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO)  unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,  Dkt.  Shabaan Mwinjaka(Kushoto) akifuatilia  moja ya mada zilizokuwa zikitolewa kwenye  mkutano  mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO)  unaofanyika mjini  Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Mgeni  rasmi  wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika, Mbwana J. Mbwana (watano kutoka Kulia) akiwa  kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza  la  Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini  Zanzibar  kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha  mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
Posted by MROKI On Thursday, October 02, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo