Nafasi Ya Matangazo

October 01, 2014



Na Fadher Kidevu Blog
KOCHA msaidizi wa Simba Selemani Matola,amesema wamerekebisha mapungufu yaliyokuwepo kwenye safu yao ya ulinzi na anauhakika watapata ushindi Jumamosi wakati watakapo pambana na Stend United kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Matola ameiambia Fadher Kidevu Blog, kuwa sare mbili mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani zimewanyima raha yeye na bosi wake Patrick Phiri, na kuamua kuyafanyia kazi ambayo anaamini itaanza kuonekana kwenye mchezo huo wa Jumamosi.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafunga mabao na hayarudishwi Jumamosi kwa sababu yale makosa yaliyokuwa yanajitokeza kwenye mechi mbili zilizopita tayari tumeyarekebisha na sasa tupo vizuri  na tunataka ubingwa,”amesema Matola.

Simba inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 2 katika mechi mbili ilizocheza katika mchezo wa kwanza ulichezwa uwanja wa taifa Septemba 21 ilitoka sare ya 2-2 na Coastal Union na mechi ya pili dhidi ya Polisi Moro ikapata sare nyingine ya 1-1 mechi zote timu hiyo ikitangulia kufunga mabao kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili mambo yanakuwa magumu na mabao yote kurudishwa.
Posted by MROKI On Wednesday, October 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo