Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2014



Na Fadher Kidevu Blog
IKIWA zimebaki wiki mbili kabla ya mahasimu wa jadi katika soka la Tanzania kukutana klabu ya Simba inaondoka kesho (Oktoba 8,2014)  kuelekea Afrika Kusini kupiga kambi ya wiki moja na nusu kujianda na pambano hilo lililopangwa kufanyika Oktoba 18 uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Wakati Simba ikienda Afrika Kusini wapinzani wao Yanga bado hawaja weka wazi sehemu gani watakapokwenda kupiga kambi kujiandaa na pambano hilo lenye upinzani mkubwa kwa soka la Tanzania.

Makamu wa Rais wa Simba Godrey Nyange Kaburu,amesema timu hiyo itaondoka na wachezaji wake wote akiwemo kipa Ivi Mapunda na watafanya mazoezi magumu ili kuweza kushinda mechi hiyo ambayo inaumuhimu mkubwa licha ya kuwa na matokeo mabaya katika mechi zilizo pita.

“Kilikitu kinakwenda sawa ikiwemo kuandaa Paspoti na viza za kuingilia Afrika Kusini matumaini yetu kambi ya Afrika Kusini itakuwa ya mafanikio na kupata ushindi kama tulivyo dhamiria,”amesema Kaburu
Simba imekuwa na mwenendo mbaya tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu na ina pointi tatu katika mechi tatu ilizocheza ikiwa nyumbani uwanja wa taifa  ambazo zote imeambulia sare.
Posted by MROKI On Tuesday, October 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo