Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2014

TAARIFA YA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime(pichani) ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08.10.2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.

Ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya dola tumeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na wote mitaani kufuatilia tukio hili muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.

Niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote  au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nao watalifanyia kazi. Pia wenye nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao na wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa polisi.

Pia wananchi wote pamoja na wageni wote watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka waliyopewa  Jeshi la Polisi.
 Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Posted by MROKI On Tuesday, October 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo