Nafasi Ya Matangazo

October 03, 2014



Na Fadher Kidevu Blog
KLABU 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara zimetishia kutotumia  jezi zenye nembo  ya mdhamini mkuu wa ligi ambaye ni Vodacom pamoja na  matangazo ya moja kwa moja ya Azam Televisheni endapo Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF itakata asilimia tano ya mgawo wa  fedha za udhamini kama ilivyoaga.

Wakili anayezisemea klabu hizo Damasi Ndumbaro ameiambia Goal kwamba klabu hazina imani na Rais wa TFF Jamal Malinzi na kutaka kuitishwa mkutano mkuu wa dharura na kumwomba Mkaguzi Mkuu wa Serikali kufanya ukaguzi  TFF ili kuangalia matumizi mabaya ya fedha.

Alisema atakayethubutu kukata makato hayo watasimamisha Ligi siku ya pili, na kutotumia vifaahivyo muhimu na katika kutekeleza hilo watawaandikia barua wadhamini hao Vodacom na Azam Televisheni kuwajulisha kinachoendelea.

Dk. Ndumbaro alisema kitendo cha Malinzi kusema Bodi ya Ligi sio chombo huru ni upotoshwaji, na  kwamba ukweli  kile  ni chombo huru kama ilivyo Kamati ya Sheria na nidhamu na kwa mujibu  ibara ya 40 kifungu kidogo cha (1) kitendo cha TFF na Kamati ya Utendaji kuingilia mamlaka ya Bodi ni ukiukwaji, mwenye mamlaka ni Mkutano Mkuu.

Alifafanua  kuwa Kamati ya Mashindano ya TFF ndio yenye mamlaka ya kuandaa kanuni na ndio waliopendekeza asilimia tano na sio Kamati ya Utendaji kama alivyobainisha Malinzi.

Pamoja na hilo, alisema Rais huyo  amepotosha  kuwa Bodi ya Ligi haina mamlaka ya kusaini mikataba ya wadhamini kisheria wakati katika mkataba wa Azam  wa mwaka 2013 kuna sahihi ya TPL, TFF na Azam Media na kuongeza kuwa mkataba ambao Malinzi aliowaonyesha waandishi wa habari ni wa mwaka 2012 ambapo Bodi hiyo ilikuwa haijaundwa.

Juzi Malinzi alisema watake wasitake lazima makato hayo yakatwe  kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya soka la vijana.
Posted by MROKI On Friday, October 03, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo