Nafasi Ya Matangazo

September 20, 2014

Kavumbagu akishangilia mechi ya jana na Polisi Moro

Na Fadher Kidevu Blog
MABINGWA wa tetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Azam FC wameanza vyema mpya wa Ligi ya Vodacom baada ya kuifunga Polisi Moro mabao 3-1 katika mechi kali iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mabao ya washindi Azam FC,katika mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji mpya aliyekuwa akiichezea Yanga msimu uliopita raia wa Burundi Didier Kavumbagu aliyefunga mabao mawili dakika za 14 na 40 huku beki Aggrey Moris akifunga bao la tatu dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza na bao la kufutia machozi la Polisi Moro limefugwa na Nahoda Bakari dakika ya 72.

Katika mchezo huo timu zote mbili zilionyesha kiwango cha juu kwa muda tofauti tofauti lakini uzoefu umewasaidia vijana wa kocha Mcameroon Joseph Omog,kuondoka na pointi zote tatu.

Matokeo ya mechi nyingine za ufunguzi zilizo chezwa leo zaligi kuu

Ndanda FC ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Kambarage Shinyana imeifunga Stend United mabao 4-1.

Na mechi nyingine Ruvu Shooting imekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Katika uwanja wa Mkwakwani Tanga Mgambo JKT imeifunga Kagera Sugar bao 1-0


na Mbeya City iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya imetoka sare ya 0-0 na JKT Ruvu
Posted by MROKI On Saturday, September 20, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo