Nafasi Ya Matangazo

September 09, 2014



Mji wa Lusail uliopo umbali wa maili 9 kutoka mji mkuu wa Doha huko Qatar ndio umepangwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Dunia mwaka 2022.

Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo makubwa duniani ya mpira wa miguu na fainali zake zimepangwa kufanyika katika mji huo tarajiwa utakao jengwa katika pwani ya Jangwa.

Qatar wapo wamesha toa michoro mbalimbali ya majengo ya Hoteli, viwanja na maeneo mengine mbalimbali ya namna mji huo mpya utakavyojengwa ili kukidhi mahitaji ya wageni katika fainali hizo.

Zaidi ya pauni bilioni 25 zinataraji kutumika kujenga uwanja wa kisasa na waaina yake wa soka hapa duniani ambao utakuwa na ukubwa wa takribani maili 28 za mraba na kuweza kumeza watu 86,000 watakao keti vitini, huu si mwingine bali ni uwanja wa ‘Lusail Iconic Stadium’.

Endapo wahandisi watakamilisha kazi hiyo kwa kiwango na ubora wa michoro kama inavyo onekana iliyotolewa mji huo utakuwa wa kipekee na kivutio kikubwa cha utalii kwa Qatar.

 Sehemu ya michoro hiyo upande gati za boti.
 Uwanja wa soka wa ‘Lusail Iconic Stadium’. utakavyo kuwa.
Mandhari ya mji huo
Posted by MROKI On Tuesday, September 09, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo