Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2014


Beki wa Simba, Nassor Chollo, (no 2) akiruka kumdhibiti mshambuliaji wa Polisi Moro, Danny Mrwanda, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mcheo huo timu hizo zimetoka sare kwa kufungana bao 1-1. Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia mchezaji wake, Emmanuel Okwi, katika dakika ya 32, na la Polisi likifungwa na Danny Mrwanda katika dakika ya 50 na kufanya matokeo kuwa 1-1.
 
Katika matokeo mengine kwa michezo iliyopigwa leo katika viwanja mbalimbali nchini, Azam FC ya Chamazi wamewalambisha Ruvu Shuting lambalamba 2-0.

Mtibwa Suger ya Turiani Morogoro wameeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwafundisha soka la ukubwani timu ngeni ya Ndanda FC baada ya kuibebnesha magunia 3 ya Sukari dhidi ya mtungi 1 wa gesi.

Vijana wa Mbeya City nao wamepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wagosi wa kaya Coast Union ya Tanga.

Wapiganaji wa akiba Mgambo Shooting nao wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wapigadebe wa Tabora, Stand United.
Posted by MROKI On Saturday, September 27, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo