Nafasi Ya Matangazo

September 30, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya Mbuzii (hawapo pichani).Katibu Mkuu leo alianza ziara yake katika kata ya Mbuzii ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya chama sehemu ambayo inahistoria kwani ilitumika kwa kufanya mikutano ya harakati za kutafuta Uhuru na ni sehemu iliyojengwa ofisi ya kwanza ya Tanu wilaya ya Lushoto.

 Wananchi wa kata ya Mbuzi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba wa ofisi ya CCM kata ya Mbuzii ,Mbuzii ndio chimbuko la TANU wilaya ya Lushoto.
 Baadhi ya mazao yanayolimwa na kikundi cha ujasiriamali Maisha Plus
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus wakati wa ziara ya Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wakazi wa kata ya Dule B wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao kabla ya kuzinduliwa kwa shina la wajasiriamali la Maisha Plus.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wajasiriamali wa Maisha Plus ambapo alizindua shina la CCM wajasiriamali wa Maisha Plus katika kata ya Dule B
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupasua mawe kwenye kambi ya Maisha Plus ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijiandaa kuukata muwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba
 Kazi na Dawa! Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila muwa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba namna ya kupiga randa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya chama baada ya kuzindua shina la Maisha Plus lililopo Dule B ,jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto.
Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mponde ambapo aliwaambia kuwa CCM ndio chama pekee kinachoweza kumaliza mgogoro wao wa miaka mingi na sasa ndio wakati umefika wa kulimaliza kabisa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijadili jambo na Mbunge wa Bumbuli Mh.January Makamba mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mponde.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mponde ambapo aliwaambia suala lao la matatizo katika kiwanda cha chai amelichukua na atarudi kwao baada ya mwezi mmoja akiwa na majibu.
  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba akihutubia wananchi wa Mponde wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Abdulkarim Jambia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Vuga akionyesha juu kadi yake ya CCM baada ya kurejea rasmi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mponde.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijionea namna mashamba ya chai yalivyogeuka vichaka . Katibu Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Posted by MROKI On Tuesday, September 30, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo