Nafasi Ya Matangazo

August 27, 2014



Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake  (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.

Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.

Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Posted by MROKI On Wednesday, August 27, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo