Nafasi Ya Matangazo

August 13, 2014


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa  (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya mbadala kwa wadau wa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam leo.  Kulia ni Meneja wa Programu wa GSMA Mobile, Ferdous Mottakin na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Towers Services Ltd, Prakash Ranjalkar.
 *******
 Kampuni ya mawasiliano ya kimataifa yenye shughuli katika nchi 20 mbalimbali Asia na Afrika, leo imeshiriki kuandaa semina ya GSMA inayofanyika Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo tarehe 12 na 13 Agosti 2014 katika hoteli ya Serena.
 
Semina hiyo ya kimataifa ya GSMA inalenga zaidi kutazama maendelea ya sekta ya Mawasiliano kwa kuangalia Zaidi mipango, mafanikio na fursa ya baadaye ya mawasiliano ya nishati mbadala rafiki kwa mazingirana yaani –green telecoms, pia itaendesha majadiliano juu ya mikakati inayowezekana kuongeza maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira (green power energy).

Semina hiyo inahudhuriwa na makampuni kutoka mataifa yapatayo 60 ikiwemo Tanzania, ambapo wanajadiliana na kubadilishana mawazo katika sekta ya mawasiano.

Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel alisema, “tunajisikia fahari sana kushiriki katika mabadiliko ya nishati ya kijani yenye lengo la kutunza mazingira ambayo yataleta faida kubwa katika jamii yetu. Ushirikiano wetu na GSMA katika kuandaa tukio hili kutatuwezesha pia kuanzisha na kuleta technolojia mpya ambapo tutachangia kwa kutoa mawazo yetu katika mijadala inayohusiana na mawasilano endelevu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla sehemu yetu ya kwa jamii (CSR)”.

“Mjadala iliyoandaliwa itajikita zaidi katika mambo yanayohusu teknolojia na maendeleo yake kama vile ufahamu kwenye teknolojia ya nishati ya jua, yaani (solar hybrid technologies) au fuel cell technology na nyingine nyingi. Baadaye, wasemaji mbalimbali wataangazia fursa za uwekezaji na miundombinu ya biashara ambazo zitaweza kunufaika na uvumbuzi huu wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala–rafiki wa mazingira kutumika kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania”.aliongeza Colaso

Akiongea katika ufunguzi rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa aliwapongeza GSMA na Airtel kwa kazi yao nzuri katika juhudi za kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano.  vile vile alishukuru sana GSMA kuipa nafasi nchi ya Tanzania kuwa muandaaji wa semina hiyo muhimu kwa mwaka huu. Pia kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano hasa kwenye swala la nishati ya kuwezesha minara nchini Tanzania, Prof. Mbarawa alifurahishwa sana na mtazamo wa fulsa hiyo ya utumiaji wa teknolojia ya nishati mbadala rafiki wa mazingira.

“kunachangamoto kubwa katika Kuanzisha na kuendeleza miundombinu kwa kizazi kipya hasa kwa nchi zetu zinazoendelea. Hivyo, tuna kila sababu ya kukaa na kushirikiana jinsi ya kutumia teknolojia mbadala ili kwa pamoja kupunguza changamoto za ukosefu wa nishati, na kuendeleza ufanisi wa huduma na uhifadhi wa mazingira utakaofaidisha Afrika katika miaka ijayo” , aliongea Mheshimiwa Mbarawa.
Posted by MROKI On Wednesday, August 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo